2 Februari 2025 - 19:04
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Michigan wanaoiunga mkono Palestina wasimamishwa kwa miaka 2

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani umesimamisha shughuli za kundi la wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina kwa muda wa miaka miwili.

Kundi hilo la wanafunzi kwa jina la Students Allied for Freedom and Equality ( SAFE) limetuhumiwa kukiuka sheria za vyuo vikuu kutokana na kufanya maandamano ya kuitetea Gaza na kulaani mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo la Palestina.

Wakati wa msimu wa machipuo uliopita, Chuo Kikuu cha Michigan kilikuwa kati ya kambi kuu za mikusanyiko ya wanafunzi wanaoiteteta na kuiunga mkono Palestina wakati yalipopamba moto maandamano ya wanavyuo nchini Marekani dhidi ya vita na mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Wakati huo, wanafunzi wengi wa vyuo vikuu na maprofesa walikamatwa, kusimamishwa na hata kufukuzwa kazi kutokana na kuitisha migomo na kufanya maandamano.

Mara baada ya kuingia White House, Rais mpya wa Marekani, Donald Trump, alisaini amri ya kukabiliana na wanafunzi na makundi yanayounga mkono Palestina katika vyuo vikuu nchini humo kwa tuhuma za chuki dhidi ya Wayahudi.

342/